Sweet music
1.Hebu tafakari kisa cha Bwana Yesu, asiyemkosa wakamwangika juu,
Haijakuwepo giza kwenye historia ya mwanadamu, Yesu 'kalia mtini.
Angewaita malaika maelfu, kumzingira tena kwa utukufu,
Lakini kwa upendo, upendo agape, akafa kifo cha aibu mti,
wanadamu tuna lipi kumlipa, ila kumpa maisha atawale,
kufanya kazi, kazi shambani mwake ndilo jukumu al'otupa
wapendwa.
2.Dhihaka na chuki, ye alistahimili, kwa upendo mwingi kafa msalabani
Mungu Muumbaji tena Mfalme wa vyote, kafa kama mtumwa pendo
ajabu.
Sweet music