Tunapaswa kuthamini utajiri wetu kwa Kristo sana hivi kwamba, tunapenda kutoa na kujitolea.

1. Uhimidiwe Bwana Mungu Baba yetu milele na milele,ukuu ni wako,na uweza,na utukufu,na kushinda,na enzi maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako,utajiri na heshima hutoka kwako wewe kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tunakutolea*2

Tulete zaka kamili ghalani ili kiwemo chakula katika nyumba ya Mungu,asema tumjaribu kwa njia hiyo Bwana wa majeshi,atatufungulia madirisha ya mbinguni na kutumwagia baraka hata isiwepo nafasi ya kutoshax2.

2. Kwani sisi tu wageni mbele za Mungu na wasafiri kama walivyokuwa baba zetu wote; ni kama kivuli siku zetu duniani wala taraji ya kukaa hapana; akiba hii yote tuliyoiweka yatoka mkononi mwake,na yeye hujaribu moyo na kupendezwa na unyofu; tutoe katika unyofu wa moyo kwa hiari yetu wenyewex2.

Recently Listened by

0 comments
    No comments found

:: / ::
::
/ ::

Queue