safi sana
1.Umekuwa nasi safarini umetuongoza tumefika salama Bwana nasi twakuhimidi, umetutendea mambo tusoweza kuhesabu tusiyofaa kamwe
Hatuna cha kukulipa kwani Bwana,Baraka zako hazikomi daima tunasema ahsante,Tumesafiri milima mabonde, visiwa tumepita, Eh Bwana twashukuru
2.Familia zetu umekuwa ngao mwokozi, umetupa afya kila siku twakushukuru, umenawirisha hata mazao yetu shambani hatufai kamwe
3.Tutumie bwana jinsi tulivyo japo wadhambi, tusamehe Bwana kila tunapokosa njia, twajitoa kwa huduma yako tawala ndani yetu, tupate kibali.
safi sana